TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO VYA HABARI
WALIOUAWA, 1. FERUZ ISMAIL ELIAS
MIKA 27, MUHA IMAMU WA MSIKITI HUO NA MKAZI WA IBANDA RELINI, 2. MBWANA
RAJAB MIAKA 40, MBONDEI MFANYABIASHARA NA MKAZI WA IBANDA, 3. KHAMISI
MPONDA MIAKA 28 DEREVA WA KIWANDA CHA SAMAKI (TFP), MKAZI WA MKOLANI,
WOTE WALIJERUHIWA SEHEMU ZA KICHWANI, SHINGONI NA MIKONONI.
ALIYEJERUHIWA NI ISMAIL ABEID @ GHATI MIAKA 13, MKURYA MWANAFUNZI WA
MADRASA KATIKA SHULE YA KIISLAMU ITWAYO JABAR HILA ILIYOKO MAENEO YA
NYASAKA ALIYEPATA MAJERAHA KICHWANI NA ANAPATA MATIBABU HOSPITALI YA
NYAMAGANA.
KUTOKANA NA HALI HIYO, WAUMINI
WENGINE WALIFANIKIWA KUKIMBIA HUKU WAKIPIGA MAYOWE YALIYOPELEKEA
WAHALIFU HAO KUKIMBIA NA KURUSHA NDANI YA MSIKITI CHUPA MBILI ZA KONYAGI
ZILIZOKUWA NA PETROLI NA TAMBI ZA MOTO, CHUPA MOJA ILILIPUKA LAKINI
HAIKULETA MADHARA MAKUBWA.
JESHILA LA POLISI LIMEWAKAMATA
WASHUKIWA WATATU KWA AJILI YA KUWAHOJI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, HUKU
MSAKO MKALI WA KUWASAKA WATU WENGINE WALIO HUSIKA KWA NAMNA MOJA AU
NYINGINE KWENYE MAUAJI HAYO UKIWA BADO UNAENDELEA. NAPENDA KUWAELEZA
WANANCHI WATULIE WAKATI TUKIENDELEA NA UPELELEZI WA TUKIO HILI, NA
NATOA WITO KWA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KWA KUTOA
TAARIFA ZA WAHALIFU WA MAUAJI HAYO ILI TUWEZE KUWAKAMATA. PIA NASHAURI
NA KUSISITIZA KUWEPO NA KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA KATIKA NYUMBA ZA
IBADA, KUMBI ZA STAREHE PAMOJA NA MITAA YAO. HII ITASAIDIA KWA KIASI
KIKUBWA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA KATIKA MAENEO HAYO.
IMESAINIWA NA:
……………………….
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni