TAKUKURU yawahamasisha wananchi kushishiriki kampeni ya LONGA NASI
Kaimu
Mkuu wa Sehemu ya Uratibu na utoaji Habari,Idara ya Elimu kwa Umma toka
Taasisi ya Kuzuia na Kupmbana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Matai Kirumbi
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaa kuhusu faida
za kampeni ya LONGA NASI iliyozinduliwa na Taasisi hiyo hivi karibuni
ikilenga kuhamasisha wananchi kushiriki vita dhidi ya rushwa kwa
kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo. Kushoto ni Afisa
Uhusiano nwa Taasisi hiyo Bi Angela Mulanduzi.
…………………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi – MAELEZO
TAKUKURU yawahamasisha wananchi kushishiriki kampeni ya LONGA NASI ili kukomesha vitendo vya rushwa hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uratibu na utoaji Habari,Idara
ya Elimu kwa Umma toka Taasisi ya Kuzuia na Kupmbana na rushwa
(TAKUKURU) Bw. Matai Kirumbi wakati wa mkutano na vyombo vya Habari.
Akizungumzia Kampeni hiyo,
Kirumbi amesema inalenga kuwajengea uelewa wananchi kuhusu mapambano
dhidi ya rushwa ili kuzuia vitendo vya rushwa .
Katika Kampeni hiyo wananchi
wanatakiwa kutoa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya rushwa au viashiria
vyake kwa kupiga namba 113 au *113# kupitia simu ya kiganjani .
Huduma hiyo inapatikana kupitia mitandao ya AIRTEL,TIGO,HALOTEL,VODACOM na ZANTEL ambapo wananchi hawatatozwa gharama yoyote.
“Taarifa 8000 zimeshapokelewa na
Taasisi yetu tangu kuzinduliwa kwa Kampeni hii na nyingi ni za wananchi
kuombwa hongo na tayari tunazifanyia kazi “alisisitiza Kirumbi.
Akifafanua kuhusu taarifa hizo
Kirumbi amesema kuwa zinaonyesha wananchi wamepokea vizuri kamapeni hiyo
iliyozinduliwa tarehe 24/5/2016 na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu
Hassan.
Katika kampeni hiyo wananchi
watajengewa ujasiri zaidi ili kuongeza ushiriki wao katika mapambano
dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa na kutoa mrejesho wa kero
zilizotatuliwa.
Matarajio ni kuongezeka kwa ubora
wa huduma za jamii kwa kuwa fedha za umma zitatumika kama ilivyopangwa
katika huduma kama vile kununua dawa.
Akizindua kampeni ya LONGA NASI
jumanne tarehe 24,Mei 2016 katika viwanja vya Mwembeyanga Wilayani
Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan
alisisitiza suala la ushiriki wa kila mmoja katika mapambano dhidi ya
rushwa nchini alisema”Tunahitaji nguvu za pamoja ili kumaliza tatizo la
rushwa nchini”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni