SERIKALI KUENDELEA KUONGEZA BAJETI KWA AJILI YA BARABARA.
By Newsroom on May 23, 2016
SERIKALI imesema itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya barabara kadri uwezo wa kifedha utakavyoongezeka.
Hayo yamesemwa leo 
Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Miko na 
Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa 
Viti Maalum. Mhe. Sophia Mwakagenda aliyetaka kujua utayari wa Serikali 
katika kukubali ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya na
 kuongeza fedha katika Bajeti ya mwak 2016/2017.
Mhe. Jafo amesema 
kwamba, Halmashauri ya Rungwe iliandaaa makisio ya bajeti ya Shilingi 
bilioni 7.9 kwa ajili ya matenegenzo ya barabara katika bajeti ya mwaka 
2016/17, hata hivyo kutokana na ukomo wa bajreti fedha zilizoidhinishwa 
ni shilingi milioni 920 ambazzo zitatumika kwa ajili ya matenegenezo ya 
barabara na ujenzi wa madaraja.
“Katika mwaka wa 
fedha wa 2015/16, Halmashauri hiyo ilitengewa shilingi milioni 870 na 
tayari Serikali imeshapeleka milioni 157.9”, alisema Mhe. Jafo.
Aliongeza kuwa, fedha
 za Mfuko wa Barabara katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/17 ni 
shilingi bilioni 247.5 ambazo endapo zingegawanywa sawa kwa Halmashauri 
zote 181 zilizopo, kila Halmashauri ingekuwa na bajeti ya shilingi 
bilioni 1.3.
Amefafanua kuwa mara 
zote mahitaji yamekuwa ni makubwa kuliko uwezo wa rasilimali fedha 
kukidhi mahitaji hayo ndiyo maana Serikali inaweka vipaumbele ili 
kutekeleza mambo machache kwanza kulingana na uwezo uliopo kibajeti.
“Serikali itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya barabara kadri uwezo wa kifedha utakavyoongezeka”, alisema Mhe. Jafo.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni