BREAKING NEWS- NDEGE YA MISRI YAPOTEA IKIWA NA ABIRIA 59 IKITOKA PARIS
Ndege
moja ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka mji
mkuu wa Ufaransa Paris hadi Cairo, imepotea kutoka kwenye mitambo ya
rada.
Maafisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A320, ilikuwa na abiria 59 na wahudumu kumi.
Shirika
hilo limesema kuwa ndege hiyo ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya
bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga ya
Misri.
Misri imetuma ndege za kivita kusaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki.
Picha kwa hisani ya msm
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni