Jamii yatakiwa kudumisha na kuenzi Utamaduni
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bi. Lily Beleko kutoka Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akisikiliza swali kutoka kwa mwandishi
wa habari (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni
yanayotarajia kufanyika Mei 21 mwaka huu.Picha na Eliphace Marwa –
MEELEZO
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bi. Lily Beleko kutoka Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akisisitiza jambo wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho
ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni yanayotarajia kufanyika Mei 21 mwaka
huu ,kulia ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw.Benjamini Sawe.
Katika kuelekea kilele cha
maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani Serikali imeitaka
jamii kuhifadhi kulinda na kuheshimu utamaduni wa nchi kwa vile ndio
kitambulisho cha Taifa letu ili kuweza kutambulika ndani na nje ya nchi.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar
es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya
Habari,utamadunu,Sanaa na Michezo Bi.Lily Beleko wakati akizungumza na
Waandishi wa habari kuhusu cha maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa
Utamaduni Duniani ambapo kauli mbiu ya madhimisho ya mwaka huu ni”
Utamaduni wa Uadilifu na Nidhamu ya Kazi Huleta Maendeleo”, “Sasa Kazi
Tu”.
Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni
Bi.Lily Beleko amesema kuwa ni wajibu kwa kila mtanzania kuheshimu
Utamaduni wetu na kushiriki kikamilifu katika kuutambua, kuujenga,
kuuendeleza na kuurithisha kwa vizazi vingine.
“Siku hii ni maalumu kwa kila
mtanzaniana na kila mmoja hana budi kukubaliana na harakati hizi za
kulinda, kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni wetu kwa ajili ya vizazi
vijavyo”Alisema Bi Lily.
Bi.Lily Beleko ameongeza kuwa
nchi haiwezi kutambulika na kuheshimika kama Taifa huru bila kuwa na
Utamaduni wake hivyo kuwepo kwa maadhimisho haya kunaipatia jamii fursa
ya kuendelea kukumbushana ,kuhamasishana na kuhimizana katika kuuenzi
utamaduni wa nchi.
Siku ya Uanuwai wa Utamaduni
Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 21 Mei, ambapo siku hiyo
imeteuliwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuona umuhimu wa kuhifadhi
na kuendeleza Utamaduni na hivyo kupitisha Azimio Na 57/249 mnamo mwaka
2002.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni