Tigo yamdhamini Ben Pol kuburudisha ‘Tamasha la Nyama Choma’
Tamasha hilo ambalo
linafanyika kwa mwaka wa tano sasa ni moja ya tamasha maarufu
linalovutia watu wengi kutoka maeneo yote ya Dar es Salaam litafanyika
kwenye viwanja vya Leaders Jumamosi Mei 28, 2016.
Akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari, Mkuu wa Tigo wa masuala ya Dijitali Paulina Shao
alisema kuwa kumuunga mkono Ben Pol kunaonesha kuendelea kujikita kwa
Tigo katika kuwekeza katika kusaidia sekta ya muziki ya ndani kwa
kuhakikisha wasanii wanawezeshwa kufikia viwango vya juu katika kazi
zao.
“Kama kampuni ya maisha ya
kidijitali, Tigo inatambua mchango muhimu wa wasanii wa Tanzania
wanaoutoa katika sekta ya burudani. Hii ndio maana tumewekeza kwa
kiwango kikubwa kuwasaidia wasanii hususani wanamuziki wa ndani
katika kuhakikisha wanafahamika katika masoko ndani ya nchi, kikanda na
kimataifa kwa kutumia majukwaa ya kidijitali yanayokuwepo na kushiriki
matukio mbalimbali na hivyo kuongeza mauzo ya muziki wao pamoja na
nembo zao,” alisema Shao.
Aidha akiishukuru Tigo kwa
uungwaji mkono huo, Ben Pol aliisifu Tigo kwa juhudi inazofanya bila
kuchoka katika kukuza ukuaji wa sekta ya muziki wa ndani kupitia
Jukwaa la Muziki la Tigo.
“Ninaishukuru sana Tigo kwa
uungwaji mkono ambao ni muendelezo wa mtiririko wa programu ambazo
imezianzisha ili kuinua maisha ya wasanii wachanga wa Tanzania,”
alisema Ben Pol na kutoa changamoto kwa wasanii wanaoibukia kuwa wasione
aibu kuomba msaada kutoka kwa mashirika kama Tigo.
Nguli huyo wa muziki wa Bongo Flava kwa hivi sasa anatamba na kibao ‘MoyoMashine’ ambayo aliitoka hivi karibuni.
Ben Pol ni miongoni mwa
wasanii wanaonufaika na jukwaa la Muziki la Tigo ambalo lilianzishwa
mwaka 2015 likiwa na lengo la kuiunga mkono sekta ya muziki Tanzania
kwa kuwasaidia wasanii wa ndani kupata kipato zaidi kutokana na mauzo
ya kazi zao na kuwawezesha kufahamika katika masoko ya kimataifa
kupitia majukwaa hayo ya kidijitali kama vile Music portal na Deezer,
ambayo ni majukwaa ya kimataifa yaliyo kwenye mtandao yakiwa na nyimbo
kutoka sehemu mbalimbali duniani zaidi ya milioni 36.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni