Serikali yawapa miezi miwili waishio kijjiji cha michezo Changamani kuhama.
Kaimu
 Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa 
na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akitoa agizo la kuhama kwa wananchi wa 
eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam(Hawapo Pichani)
 kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
Kaimu
 Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa 
na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisistiza jambo mbele ya wajumbe wa kikao
 kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke 
jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao 
kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha 
Michezo.
Kaimu
 Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya akichangia hoja katika kikao
 kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke 
jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao 
kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha 
Michezo.
Mwakilishi
 wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Mafuku Rajabu akifafanua jambo katika 
kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya 
Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi 
hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha 
Michezo.
Eneo
 la Changamani kijiji cha Michezo ambalo wananchi wake wanatakiwa kuhama
 ndani ya miezi miwili kupisha uendelezwaji wa eneo hilo kwa ajili ya 
michezo mbalimbali.
Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM
………………………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi WHSUM.
Serikali imewapa miezi miwili 
wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha Changamani kilichopo 
Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam  kuhama katika eneo hilo kupisha 
uendelezwaji wa kijiji cha mchezo.
Agizo hilo limetolewa na Kaimu 
Mkurugenzi Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na 
Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipokutana na wananchi hao katika kikao cha 
kujadili na kukubaliana muda wa kuhama katika eneo hilo leo Jijini Dar 
es Salaam.
“Ndugu zangu tumejadiliana wote 
na kukubaliana kuwa baada ya miezi miwili mtakuwa mmeshaama katika eneo 
hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha michezo kwa ajili ya shughuli za
 mbalimbali za michezo” alisisitiza Bw. Nkenyenge.
Naye Kaimu Meneja wa Uwanja wa 
Taifa Bw.Julius Mgaya amesema kuwa mpango wa kuwahamisha wananchi hao 
unalenga kutekeleza mradi wa kijiji cha michezo kitakachojengwa kwa 
ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali.
Kwa upande wake mmoja ya 
wawakilishi wa wananchi hao Bw.Atillio Mballa amesema wamekubaliana na 
muda huo waliopewa na watafikisha ujumbe huo kwa wenzao na kabla ya muda
 hujafika watakuwa wameshatekeleza agizo hilo.
Katika mpango wa kukuza na 
kuendeleza michezo nchini Serikali imejipanga kukuza sekta ya michezo 
nchini na kuifanya kuwa moja ya rasilimali itakayochangia katika pato la
 taifa.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni