Ijumaa, 20 Mei 2016

WASIFU WA BRAZIL NA URUGUAY KABLA YA MICHUANO YA COPA AMERICA ITAKAYORUSHWA LIVE NA STARTIMES

ura1Ni taifa lenye kuongoza kwa rekodi nyingi katika historia ya Kombe la Dunia. Ndio taifa pekee lililoshiriki fainali za Kombe la Dunia bila kukosa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930. Na ndio taifa lenye kushikilia rekodi ya kulitwaa kombe hilo mara tano
Ni taifa lenye kuongoza katika marathoni ya rekodi ya kombe hilo, kwa kuongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi kwenye mechi za Kombe la Dunia. Wanaongoza kwa kushinda mechi zaidi kuliko taifa lingine lolote kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Dunga tayari ameshatangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Copa America kwa mwaka 2016, likiwa jina la Neymar halipo katika list hiyo ya majina 23, Neymar anakosekana katika list hiyo kutokana na FC Barcelona kuomba asiitwe staa huyo kwa ajili ya michuano hiyo.
Hawa ndio watakaoshiriki kuchezea kombe hilo mwaka huu. Magoikipa: Alisson (Internacional), Diego Alves (Valencia) and Ederson (Benfica), Mabeki: Daniel Alves (Barcelona), Fabinho (Monaco), Filipe Luis (Atletico Madrid), Douglas Santos (Atletico Mineiro), Miranda (Inter Milan), Gil (Shandong Luneng), Marquinhos (Paris Saint-Germain), Rodrigo Caio (Sao Paulo)
Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Elias (Corinthians), Casemiro (Real Madrid), Rafinha (Barcelona), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Liverpool), Lucas Lima (Santos) na Willian (Chelsea). Washambuliaji: Douglas Costa (Bayern Munich), Hulk (Zenit), Ricardo Oliveira (Santos) na Gabriel (Santos)
‪#‎CopaAmericaOnStarTimes ‪#‎Exclusive Ni taifa lenye kuongoza kwa rekodi nyingi katika historia ya Kombe la Dunia. Ndio taifa pekee lililoshiriki fainali za Kombe la Dunia bila kukosa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930. Na ndio taifa lenye kushikilia rekodi ya kulitwaa kombe hilo mara tano
ura2Uruguay imekuwa moja kati ya timu za taifa ambazo zinatajwa kuwa bora zaidi duniani. Na historia yao ilijijenga baada ya kutwaa taji la kombe la dunia mara mbili kwa mtindo wa aina yake mwaka 1930 na mwaka 1950. Baada ya kushindwa kufuzu kwenye michuano ya mwaka 1994 nchini Marekani na mwaka 1998 nchini Ufaransa timu ya taifa ya Uruguay “La Celeste” ilirejea kwenye michuano ya mwaka 2002 nchini Japan na Korea na kutolewa kwenye hatua ya makundi. 
Tukiingia katika Copa America Uruguay naweza kusema ndio inaongoza katika ubingwa kwenye michuano hii, ilishinda kombe hili mara 15, na mara ya mwisho ilichukua mwaka 2011.
Pia walishinda medali mbili za dhahabu katika mashindano ya summer Olympics. Kabla ya kuundwa kwa kombe la dunia Uruguay walinyakua kombe la Mundialito mwaka 1980. Mpaka sasa Uruguay imeshinda  vyeo 20 rasmi , kwa rekodi ya dunia kwa majina ya kimataifa uliofanyika kwa nchi zote Je katika michuano hii, itafanikiwa kuchukua ubingwa? ‪#‎CopaAmericaOnStarTimes ‪#‎Exclusive 
Download APP ya StarTimes sasa na uweze kujishindia zawadi kem kemwww.startimes.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni