HESHIMA YA KOCHA, WACHEZAJI LEICESTER SASA YAHAMISHIWA KWENYE KUTA ZA MJI WA LEICESTER
Heshima ya mashujaa walioipa Leicester City ubingwa wa Ligi Kuu England sasa itabaki milele.
Mashujaa
 hao, kuanzia Kocha Claudio Ranieri na wachezaji wengine, picha zao 
zimeanza kuchorwa katika kuta za mitaa mbalimbali za mii wa Leicetster.
Wachezaji
 ambao tayari mchoraji maarufu Richard Wilson ameanza kuwachora ni 
nahodha Wes Morgan,kipa Kasper Schmeichel na mwanasoka bora wa mwaka wa 
Ligi Kuu England, Riyad Mahrez.
Imeelezwa, mchoraji huyo maarufu atawachora wachezaji wote lakini akianza na kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
 








 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni