WEMA AZINDUA MOBILE APLICATION YAKE, HABARI ZAKE ZITAPATIKANA HUMO
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na Miss
Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini Wema Sepetu
wakifunua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa Wema Sepetu Mobile
Application ya msanii Wema Sepetu kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini
Dar es salaam jana , Katika Aplication hiyo kutapatikana habari
mbalimbali za msanii huyo mwigizaji wa filamu pamoja na habari
zinazohusu masuala mbalimbali ya kazi zake hii ni kwa mara ya kwanza
katika nchi za Afrika Mashariki kwa msanii kuwa na Mobale Aplication
yake hivyo msanii mwingine atakayekuja atakuwa anafuata nyayo za Wema
Sepetu.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia
wakati wa uzinduzi wa Wema Sepetu Mobile Application ambapo alimpongeza
Wema kwa hatua kubwa aliyofikia ya kuwa msanii wa kwanza wa Filamu
nchini kuwa na Mobile App na kuwataka wasanii wengine kuwa wabunifu na
kuja na mipango ambayo itawanufaisha zaidi.
Msanii wema Sepetu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mobale Aplication yake kwenye hoteli ya Hyyat Regency.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimpongeza
msanii Wema Sepetuwakipiga picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Mtaalamu wa Mobile Application Ndugu Haji Yussuf akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wema Sepetu Mobile Application
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza
jambo na Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini Wema
Sepetu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
akipiga picha ya pamoja na Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa
Filamu nchini Wema Sepetu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipiga picha ya pamoja na Miss Tanzania 2006 na Muigizaji maarufu wa Filamu nchini Wema Sepetu na mama yake kushoto pamoja Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Hartman Traders Ndugu Cecil na Mtaalamu wa Mobile Application Ndugu Haji Yussuf wa pili kutoka kushoto wakati wa uzinduzi wa mobile Application yake ambayo itawasaidia wapenzi na mashabiki wake kupata habari sahihi na za uhakika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni