TUHUMA DHIDI YA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KUHUSU UTAFUNAJI WA MAMILIONI YA FEDHA
Tunapenda kufafanua kuwa taarifa
za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinaeleza kuwa,
Chuo cha Usimamizi wa Fedha kilipokea fedha za ziada kutoka Wizara ya
Fedha kwa ajili ya mishahara na fedha hizo zilishapangwa kurudishwa
ndani ya mwaka wa fedha 2015/2016 kama ripoti ya Mkaguzi ilivyoagiza
katika mwaka wa fedha wa 2014/2015. Kwa hiyo fedha hizo hazijatafunwa
wala kupotea.
Kuhusu ukusanyaji wa madeni
yaliyoripotiwa, nusu ya deni ni karo ya wanafunzi wanaolipiwa na Bodi ya
Mikopo na fedha hiyo ililipwa Chuoni ndani ya mwaka wa fedha 2014/2015.
Madeni mengine ni ya wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo kwa
sababu mbalimbali na madeni hayo yanafutwa kwa kufuata taratibu za
kifedha (Financial Regulation) kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu
za serikali alivyoelekeza.
Ufanunuzi huu ulitolewa kwa
mwandishi wa gazeti hili (Bwana Gabriel Mushi) mnamo tarehe 04-05-2016
alipoongea na Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala.
Kwa kumalizia Chuo cha Usimamizi
wa Fedha kinafanya kazi zake kwa kufuata taratibu zilizowekwa na kwa
zaidi ya miaka 30 mfululizo Chuo kimepata hati safi za mahesabu (Clean
Audit Report) kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za
Serikali (CAG).
Taarifa hii imetolewa na
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni