Jumatatu, 30 Mei 2016

indexMratibu Miss Chang’ombe 2016 kutoka  Kampuni ya SG Entertainment Adam Hussein(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa Mashindano ya Urembo Kitongoji cha Chang’ombe yanayotarajiwa kuzinduliwa Juni 02, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa kampuni hiyo Victor Mkumbo na Kulia ni Meneja Masoko Geofrey Msala.(Picha Na: Lilian Lundo)
 Kampuni ya SG Entertainment kuzindua mashindano ya urembo ya Miss Chang’ombe Juni 2, 2016 katika Ukumbi wa MPOA AFRIKA uliopo Davis Corner Tandika jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa kampuni hiyo Victor Mkumbo  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza  kuwa  watakaoshiriki mashindano hayo ni wakazi wa Chang’ombe na Temeke peke yake.
“Washiriki wa mashindano haya ni wakazi wa Chang’ombe na Temeke, nje ya hapo haturuhusu mtu kutoka eneo lingine kushiriki, lengo ikiwa ni kuwapa fursa wakazi wa maeneo haya”,” anasema Mkumbo.
Kwa upande wake Mratibu wa Miss Chang’ombe 2016 Adam Hussein anasema kwamba nafasi za warembo kushiriki bado zipo na fomu za kujiunga zinapatikana CDS PARK(TCC Club) Chang’ombe, MPOA AFRIKA Davis Kona na duka la nguo CHILU Latest Wear Temeke Mwisho kwa gharama ya shilingi 5,000 tu.
Aliongeza kuwa fainali ya mashindano hayo itafanyika Julai 21, 2016 katika viwanja vya CDS Park(TCC Club) Chang’ombe ikisindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Galatone ,mwadada  Chemikal.
Washindi watano kutoka Kitongoji cha Chang’ombe wataungana na warembo kutoka vitongoji vya Kigamboni na Mbagala ili kutafuta warembo wa Temeke watakao wakilisha katika mashindano ya kitaifa ya kumtafuta mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Mrembo wa Dunia mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni