DRFA,YAJIVUNIA KLABU ZAKE KUMALIZA MSIMU 2015/2016 KWENYE NAFASI ZA JUU.
Chama cha soka mkoa wa Dar es
salaam DRFA imezipongeza klabu zake tatu za ligi kuu kwa kumaliza katika
nafasi za juu kwenye michuano ya ligi kuu soka tanzania bara.
Timu hizo ni Yanga SC iliyomaliza
katika nafasi ya kwanza,Azam FC iliyomaliza katika nafasi ya pili na
Simba SC iliyomaliza katika nafasi ya tatu.
amesema mafanikio hayo
wanayapeleka moja kwa moja kama zawadi kwa mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam Mh .Paul Makonda,ambaye ameonesha mchango mkubwa kwa kuhimiza
watu kupenda michezo.
Amesema kama chama hawana budi
kujivunia mafanikio hayo na kuwapongeza wachezaji,walimu na viongozi wa
vilabu vyote vitatu kwa hatua hiyo inayozidi kuupamba mkoa wa Dar es
salaam kisoka.
MAKUMBUSHO,SIFA POLITAN,ZIMA MOTO ZATAKIWA KILA LA KHERI LIGI ZA MIKOA.
DRFA,inazipongeza timu za
Makumbusho FC,Sifa Politan na Zima Moto kwa kufanikiwa kuingia katika
ligi za mikoa baada ya kufanya vizuri katika michezo yao.
Klabu ya Zima Moto itakwenda kucheza mkoani Njombe,wakati Makumbusho na Sifa Politan wanakwenda kucheza mkoani Morogoro.
Pia klabu ya Abajalo FC nayo
imepongezwa kwa mafanikio ya kutinga ligi daraja la kwanza,na kuwataka
kuzidisha mapambano ili wapige hatua nyingine zaidi ya kufika ligi kuu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni