TAARIFA KUTOKA TFF
CAF YAMTEUA MICHAEL WAMBUR
Shirikisho la Soka Barani Afrika 
(CAF), limemteua Michael Richard Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa 
kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na 
Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016.
Wambura ambaye amewahi kuwa 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri 
katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. Msumbiji 
iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.
TAIFA STARS KWENDA KENYA KESHO
Kikosi cha timu ya soka ya 
Tanzania – Taifa Stars, chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na 
Hemed Morocco kinatarajiwa kuondoka kesho saa 12.00 alfajiri kwenda 
Nairobi, Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa 
kimataifa
Mchezo huo ni maandalizi ya 
kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kucheza 
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia 
itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni