Waziri Profesa Makame Atembelea daraja la Nyerere na Kituo cha kupimia mafuta yaingiayo nchini kuona Maendeleo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
 Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey 
Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo 
kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es 
salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji.
Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)
 Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa 
kujenga fly overs katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza 
msongamano wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka 
Kampuni ya Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
 Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto 
wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo
 jijini Dar es salaamu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
 Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo  kutoka kwa Fundi mitambo Bw. 
Simon Dotto  kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta 
kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki ambao uliharibika 
hivi karibu kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
 Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo  kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa
 kivuko cha Mv Magogoni kuhusu utaratibu wa ukatishaji tiketi katika 
kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
 Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo na changamoto mbalimbali kutoka 
kwa abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni leo jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Beatrice Lyimo)
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni