WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI DART LEO
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
 na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi 
ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi 
Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa 
DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu 
ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali 
zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili 
ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi. 
Usafiri DART  umekuwa  mkombozi 
kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani 
mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani  aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia 
jambo wakati Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa akisamimiana na Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani  aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
Baadhi ya abiria wakisafiri pamoja na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kwenye basi la DART.
Moja ya Basi likiwa katika ruti yake kutoka Kimara kuelekea Posta.
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikagua 
kituo cha Kimara Mwisho mara baada ya kuwasili kituoni hapo
Moja ya basi la Mwendo kasi likipakia abiria katika kituo cha Kimara Mwisho leo.
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
 na mwanafunziambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati alipofika
 kwenye kituo cha mabasi ya Mwendo kasi Kimara Mwisho leo.
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiuliza 
swali kwa mmoja wa wafanyakazi wanaokatisha tiketi katika vituo hivyo 
wakati alipokagua miundombinu ya DART leo.
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiangalia 
utendaji kazi unavyoendelea ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto 
zinazojitokeza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikaua kituo cha Kimara Mwisho.
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia 
jambo na Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa katikati ni Mzee David 
Mwaibula.
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
 na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundombinu hiyo leo kulia
 ni Mzee David Mwaibula na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama 
Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni