SHUKURANI TOKA KWA FAMILIA YA ANKAL KUFUATIA MSIBA WA MWANAE MAGGID
Familia
ya Ankal Muhidin Issa Michuzi inapenda kutoa shukrani nyingi sana
sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa
kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae
Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki
iliyopita na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu
mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu
alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi.
Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya
shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote
ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.
Pamoja na hayo shukrani za
kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na
Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote,
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake
yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama
Anna Mkapa na familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde
Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Allan
Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu
Mhe. Ombeni Sefue pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba mfiwa kwa
kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa kila kitu
katika msiba huu kinaenda sawasawa. TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA
ZAKE ZOTE…
Salamu zingine za kipekee
ziwaendee watumishi wote wa Ubalozi wetu Afrika kusini mjini Pretoria
ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa wa Ubalozi kaka
Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban kuja
Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA…
Vile vile shukrani za kipeke
ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban
pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha
mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima
zote. ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO…
Kwa Uongozi wa msikiti wa
Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani za
kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kidini
katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa watovu wa fadhila
endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote
ambayo baba mfiwa Ankal ni mwanachama. Shukurani hizi maalum ziwaendee
Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old
Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari,
Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The
Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia,
Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania
Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists
TZ, PPAT Members, P Mamas, RUBY 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group,
Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote
katika Social media wakiongozwa na Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya
Marekani. TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA KWA MICHANGO YENU YA HALI
NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA…
Mwisho, lakini sio kwa
umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa
shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa
marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia
logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
Dar es salaam.
HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA
KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA
WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE…
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji’un
AMIN!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni