MSANII SNURA MUSHI AOMBA MSAMAHA MBELE YA WATANZANIA KWA VIDEO YAKE YA ”CHURA” KUKIUKA MAADILI YA KITANZANIA
Msanii
wa kizazi kipya Snura Mushi (kulia) akiomba msamaha mbele ya Watanzania
kutokana na kusambaza video yake iliyokiuka maadili ya Kitanzania
maarufu kama ”Chura” mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi wa kazi zake Bwana Hemed Kavu
maarufu kama HK.
Msimamizi
wa kazi za Snura Mushi Bwana Hemed Kavu maarufu kama HK (kushoto)
pamoja Msanii wa kizazi kipya Snura Mushi wakionyesha Cheti
alichokabidhiwa Bi Sunra Mushi na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa
ajili ya kuruhusiwa kufanya kazi zake za kisanaa nchiniPICHA ZOTE NA
BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
.…………………………………………………………………………………………………
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
Dar es Salaam
Msanii wa kizazi kipya Snura
Mushi amewaasa wasanii nchini kujisajili katika mamlaka zote
zinazosimamia kazi za sanaa ili waweze kuzingatia sheria na kanuni
zilizowekwa, kutambulika na kuiendeleza tasnia ya Sanaa nchini.
Ameyasema hayo leo jijini Dar
es salaam alipokuwa akiomba radhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania hasa sekta zinazosimamia Sanaa nchini na Watanzania kwa ujumla
kwa kutokufuata Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa
Sanaa nchini.
“Tunaomba radhi kwa Serikali,
Umma na Watanzania kwa ujumla kwa kosa la kutengeneza, kuzindua na
kuweka mtandaoni Video ya udhalilishaji wa wanawake na isiyozingatia
maadili ya kitanzania ya muziki unaoitwa Chura” alisema Msanii huyo
Aidha Msanii huyo ameahidi kuwa
mfano katika jamii na kwa wasanii wenzake katika masuala yahusuyo
kutunza na kufuata maadili na utamaduni wa kitanzania pamoja na sheria
za nchini.
Mbali na hayo ameahidi
kutekeleza maazimio na maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, BASATA na mamlaka ya Mawasiliano (TCRA)
kuhusu video ya chura, ambayo ni kuitoa video ya Chura kwenye mtandao wa
You Tube, kujisajili BASATA na kuifanya upya video hiyo.
Aprili 4, 2016 Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliifungia video ya muziki wa Chura
kutokana na video hiyo kumdhalilisha mwanamke pamoja na tasnia ya muziki
kwa kutozingatia maadili na utamaduni wa mtanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni