LUHWAVI ATEMBELEA WAJUMBE WA MASHINA WILAYANI KIBAHA
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajabu Lhwavi akisalimiana na Mjumbe wa Shina
namba tisa, tawi la KKKM, Kata ya Picha ya Ndege, Wilayani Kibaha mkoa
wa Pwani, Bibie Lukemo, alipotembelea shina hilo, jana, kukagua uhai wa
chama akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo. Katikati ni Mwenyekiti
wa CCM Kata ya Picha ya Ndege. Mwalimu Mohammed Lukemo
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi na Katibu wa CCM mkoa wa Pwani,
Joyce Masunga, wakikagua daftari la wageni, walipokuwa nyumbani kwa
amjumbe wa shina namba tatu, Tawi la Twende Pamoja, Kata ya Sofu,
wilayani Kibaha mkoa wa Pwani, Gasper Gama (kulia), Luhwavi
alipotembelea shina hilo kukagua na kuimarisha uhai wa Chama, jana.
Mjumbe
wa Shina namba tisa, tawi la CCM KKKM, kata ya Picha ya Ndege Kibaha
mkoa wa Pwani, Bibie Lukemo, akisoma taarifa ya shina hilo, Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi alipotembelea shina hilo
kuimarisha na kukagua uhai wa chama jana.
Katibu
wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga, akipanda mti wa kumbukumbu katika
eneo maalum ambalo viongozi wanaotembelea shina namba tisa, tawi la
KKKM, Kata ya Picha ya Ndege kupanda mti kama huo, alipofika na Naibu
Katibu Mkuu wa CCM- Bara, Rajabu Luhwavi, kwenye shina hilo, jana
kukagua uhai wa Chama.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajabu Luhwavi akipanda mti wa kumbukumbu
katika eneo maalum ambalo viongozi wanaotembelea shina namba tisa, tawi
la KKKM, Kata ya Picha ya Ndege kupanda mti kama huo, alipofika kwenye
shina hilo, jana kukagua uhai wa Chama.
(Picha na Bashir Nkoromo).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni