Jumatatu, 16 Mei 2016

By Newsroom on May 17, 2016
Wananchi na Wakazi wa Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, mapema leo wamefunga barabara ya Mwanza-Musoma katika eneo la Kisesa na hivyo kusababisha abiria wanaoingia Jijini Mwanza kutoka Mikoani kukwama barabarani kwa zaidi ya masaa manne.
Wamechukua maamuzi hayo baada ya dereva wa daladala moja kuwagonga wanafunzi wawili wa shule ya msingi Isangijo na kusababisha mmoja kufariki dunia papo hapo.
Baada ya hatua hiyo, jeshi la polisi, kikosi cha kuzuia ghasia limefika eneo la tukio na kuwasihi wananchi kufungua barabara hiyo ili kutowakwamisha abiria kuendelea na safari zao.
Picha na Mdau @BMG 

Wananchi wakiwa wamefunga barabara ya Musoma-Mwanza, katika eneo la Kisesa baada ya daladala kuwagonga wanafunzi wa shule ya msingi Isangijo katika eneo hilo.
Askari wa kutuliza ghasia wakia eneo la tukio
Askari wa usalama barabarani wakiwa eneo la tukio wakijaribu kuondoa mawe barabarani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni