TAASISI ZA SERIKALI ZILIZOUNGANISHWA NA MFUMO WA ITIFAKI YA INTANETI ZATAKIWA KUTUMIA HUDUMA HIYO KUPUNGUZA GHARAMA YA MAWASILIANO.
Mtaalam wa TEHAMA katika moja ya Ofisi za Serikali akiwa kazini.
Serikali
kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) imezitaka
taasisi zote zilizounganishwa kwenye mfumo wa simu zenye itifaki ya
intaneti (Internet Protocol (IP) ambazo zinatumia intaneti
kuzitumia simu hizo katika mawasiliano yao kila siku ili kuboresha
utendaji kazi na kupunguza gharama za mawasiliano Serikalini.
Meneja
Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshakangoto
amesema kuwa Serikali imeamua kusisitiza matumizi ya simu hizo ili
kuziwezesha taasisi za Serikali kuwa na mawasiliano yaliyo bora, salama
na kupunguza gharama za mawasiliano.
Amesema
kuwa Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) imeunganisha
taasisi za Serikali 72 ambazo zinajumuisha Wizara, Idara zina
zojitegemeana na Wakala za Serikali na kuongeza kuwa taasisi hizo
zimeunganishwa na Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali yaani ‘Government Communication Network (Govnet)’ unaowezesha mfumo wasimu hizo kufanya kazi kwa ufanisi.
“
Kupitia mfumo wa simu hizi zenye itifaki ya intaneti mtumishi wa
taasisi iliyounganishwa anaweza kupiga simu kwenda taasisi nyingine ya
nje ikawa kama amepiga simu ya ‘extension’ ndani ya ofisi moja” Amesema
Bi. Suzan.
Aidha,
amesema Taasisi za umma zitanufaika moja kwa moja na simu hizo kwa
kuwa, taasisi hizo zitaweza kubadilisha na taarifa kupitia mtandao mmoja
tuwa Mawasiliano wa Serikali kwa usalama na uhakika. Pia simu hizo
zitawawezesha watumishi wa taasisi mbalimbali kufanya mkutano kwa njia
ya simu wakiwa kwenye ofisi zao na hivyo kuokoa muda na gharama za
usafiri.
Hata
hivyo amesema taasisi za umma zilizopo katika mtandao wamawasiliano wa
Seikali zitaendelea kuwasilia na na taasisi zilizo nje ya mtandao huo
kwa kupitia mtoa huduma wa simu za mezani (PSTN Provider) kama vile
TTCL.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni