STARS HADHARANI MEI 18
Kocha
Mkuu wa timu ya soka Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa
Mei 18, 2016 atarajiwa kutangaza kikosi cha wachezaji wake wakaokwenda
Kenya kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini
Nairobi, Mei 29, 2016.
Taifa Stars, itatumia mchezo huo
utakaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) katika rekodi
zake, pia utatumiwa na kikosi cha Mkwasa kujiandaa dhidi Mapharao wa
Misri katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Africa (AFCON). Taifa Stars na Misri zinatarajiwa kuumana Juni 4, 2016
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni