SERIKALI YATENGA TSH MILIONI 430 KUFANYA UPEMBUZI YAKINIFU BARABARA YA TARIME- NYAMWAGA- MUGUMU
Na Ismail Ngayonga -MAELEZO -Dodoma
SERIKALI
katika mwaka 2016/17 imetenga kiasi cha Tsh. Milioni 430 kwa ajili ya
upembuzi yakinifu na usanifu wa barabara ya Tarime-Nyamwaga- mugumu
ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.
Aidha Serikali pia imetenga kiasi cha Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mara katika barabara ya Tarime-Nyamwaga-Mugumu.
Akijibu
swali la Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA), Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alisema kwa kutambua
umuhimu wa barabara hiyo hususani katika sekta ya utalii, Serikali
imekusudia kuijenga barabara hiyo kwa awamu.
Alisema
barabara hiyo imeanza kujengwa kutoka Tarime kuelekea mugumu, ambapo
hadi sasa jumla ya kilometa 6 za barabara hiyo zimekamilika kwa kiwango
cha lami katika eneo la Tarime mjini.
Aidha Mhandisi Ngonyani alisema ujenzi wa kilometa 2 unaendelea na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015/16.
“Barabara ya
Tarime-Nyamwaga- Mugumu (Serengeti) ni barabara ya mkoa yenye urefu wa
kilometa 86 ni kiungo muhimu sana kiuchumi na kijamii kwa Wilaya za
Tarime na Serengeti” alisema Ngonyani.
Katika swali
lake, Mbunge Heche alitaka kufahamu Serikali itaijenga lini barabara ya
Tarime-Nyamwaga- Serengeti kwa kiwango cha lami.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni