JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA KINGA NA TAHADHARI YA MAJANGA YA MOTO
Koplo
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuonyesha
mwananchi aliyetembelea Banda la Maonyesho la jeshi hilo jinsi ya
kutumia mtungi wa kuzimia moto wa awali, katika maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na
Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi
Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idd Chanyika (kulia) akitoa
maelezo jinsi ya vifaa vya kinga na tahadhari vinavyotumika kwa Kamishna
wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Michael Shija (kushoto), Kamishna wa
Oparesheni, Rogatius Kipali (wapili kushoto) na Naibu Kamishna wa
Utawala naFedha, Billy Mwakatage walipotembelea banda hilo Kituo cha
Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Koplo
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuandikia
mmoja ya mwananchi namba ya dharura 114 ambayo hutumika kupokea taarifa
ya majanga mbalimbali kutoka kwa jamii.
Kamishna
wa Oparesheni, Rogatius Kipali akisisitiza ufanyaji kazi kwa bidii,
nidhamu, uadilifu na weledi kwa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
wa Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam katika
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi waUumma inayofanyika katika viwanja vya
Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala, jijini Dar es Salaam.
Banda
la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lililotumika kutoa elimu ya kinga na
tahadhari ya majanga ya moto na maokozi lililopo katika viwanja vya
Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Godfrey Peter, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni