BAADA YA MIAKA 29, HATIMAYE GIGGS AAMUA KUONDOKA MANCHESTER UNITED
Si unamjua Ryan Giggs? Ameamua kuondoka Manchester United baada ya kuitumikia kwa miaka 29 akiwa mchezaji na kocha msaidizi.
Giggs anaondoka baada ya kukataa ofa ya kuwa kocha msaidizi chini ya Kocha Mpya, Jose Mourinho.
Kabla, amekuwa kocha msaidizi chini ya makocha wawili David Moyes na Louis van Gaal ambaye alifanikiwa kubeba Kombe la FA.
Giggs
,44, alijiunga Man United mwaka 1987 akiwa ndiyo anasherekea siku yake
ya kuzaliwa wakati akitimiza miaka 14. Alitokea timu ya watoto ya
Manchester City.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYhQPR0iBxnAe_pemCMscu3TxxAPtjXnL8XpGKjRXjK9Xz-vP3K-GeOVPA6o7poDYa9d7b5htFpsWKoildBkqWg_oxZ0sGG33BwIWukv2vY4O9mvEfpssm5-A-OPHYPlV1Gr60HDyjAKY/s640/article-3666675-35CC502A00000578-502_964x390.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni