 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri 
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu katika tukio la 
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa 
habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri 
Jijini Dodoma. Katika tukio hilo Dk. Tulia Ackson alichangia kiasi cha 
shilingi milioni moja.
|  | 
| Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri 
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto), Msanii wa 
Bongo Movie, Aunt Ezekiel (kulia) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian 
Kamazima (katikati) wakiosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine 
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa 
habari nchini. | 
|  | 
| Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo 
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) 
akiosha gari na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kushoto) 
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa 
habari nchini. Katika tukio hilo Dk. Hamisi Kigwangalla alichangia 
shilingi milioni moja. | 
|  | 
| Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo 
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiosha gari 
katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya 
waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa 
Jamhuri Jijini Dodoma. | 
|  | 
| Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri 
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kulia) akiosha moja 
ya magari ya wabunge kuwaunga mkono waandishi wa habari katika tukio la 
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa 
habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri 
Jijini Dodoma. | 
|  | 
| Mwenyekiti wa Bunge Sports, 
William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kuwapongeza 
waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car 
Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kulia ni Naibu
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson 
Mwansasu na Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari 
‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson (katikati). Katika zoezi 
hilo Ngeleja alichangia shilingi laki moja huku timu ya bunge ikichangia
 shs milioni moja. | 
|  | 
| Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa 
Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin 
Thompson (katikati) akizungumza katika zoezi la kuosha magari kwenye 
kampeni maalumu ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash 
For Health’ ikiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia 
bima ya afya waandishi wa habari nchini. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge 
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson na Mwenyekiti wa 
Bunge Sports, William Ngeleja (kushoto). | 
|  | 
| Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri 
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kulia) 
akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi
 wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri 
Dodoma. Dk. Tulia alichangia shs milioni tano. | 
|  | 
| Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri 
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto) akiosha 
moja ya magari ya wabunge kuwaunga mkono waandishi wa habari katika 
tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi
 wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri 
Jijini Dodoma. | 
|  | 
| Mmoja wa wasanii wa muziki 
akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine kuchangisha
 fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. | 
|  | 
| Mmoja wa wasanii wa muziki 
akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine kuchangisha
 fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. | 
|  | 
| Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo 
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) 
akimkabidhi hudi ya shs milioni moja Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa 
Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin 
Thompson (kushoto) kwa ajili ya kuchangia fedha kuwakatia bima ya afya 
waandishi wa habari nchini. Kulia ni Mratibu wa zoezi hilo. | 
|  | 
| Miss Tanzania 2014/15, Lilian 
Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa
 Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kushoto) wakijitolea kuosha magari
 kwenye kampeni hizo. NHIF waliosha gari lao kwa shs 100,000/-. …………………………………………………………………………….
 Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
 Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki harambee ya 
kuchangia waandishi wa habari kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya “Media
 Car Wash For Health” iliyofanyika leo katika viwanja vya Jamhuri Mjini 
Dodoma ambapo amechangia jumla ya shilingi milioni 5 ili kuokoa maisha 
ya waandishi wa habari.
 “Kuna umuhimu mkubwa wa kuwachangia waandishi wa habari kwani
 wamekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya nchi na 
kuhamasisha amani ya nchi, kwa kutambua umuhimu wao nitachangia shilingi
 5,000,000 ili iweze kuwakatia Bima ya Afya,” alisema Mhe.Dkt. Tulia.
 Licha ya kuchangia fedha hizo Mhe. Tulia aliosha baadhi ya 
magari ya waheshimiwa wabunge kwa ajili ya kuchangia harambee hiyo 
ambapo kila mbunge aliyeoshewa gari yake alichangia shilingi 100,000 
ambazo moja kwa moja ziliingia katika mfuko wa kuokoa maisha ya 
waandishi wa habari kwa kuwakatia Bima ya Afya.
 Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendelea ya Jamii, 
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla amechangia shilingi 
1,000,000/= ambayo nayo inaenda kusaidia waandishi wa habari ili waweze 
kukatiwa Bima ya Afya.
 Lengo la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni
 200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima ya afya zaidi ya  waandishi wa 
habari 1000 hapa nchini.  Aidha harambee hii ni ya pili, harambee 
nyingine kama hii ilifanyika mwaka 2015, viwanja vya Leaders jijini Dar 
es Salaam na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidia 
kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa wanaugua kwa kipindi 
kirefu.
 | 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni