siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu zangu waandishi wa habari,
Leo tarehe 30.6.2016 ndiyo tarehe 
na siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha. Kwa mujibu wa takwimu za 
silaha tulizonazo inaonyesha kwamba wapo baadhi ya wamiliki wa silaha 
ambao hawajatekeleza agizo la kuhakiki silaha wanazozimiliki.
Kufutia hali hiyo, natoa angalizo 
kwa wale wote ambao hawajahikiki silaha zao kwamba muda wowote kuanzia 
sasa tutaanza operesheni maalum ya kutafuta silaha ambazo 
hazijahikikiwa.  Ifahamike kwamba yeyote atakaye kutwa na silaha ambayo 
haijahakikiwa atachuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo  kupoteza sifa 
ya kuwa mmiliki halali wa silaha hiyo.
Tunatoa agizo kwa wamiliki binafsi
 wa maghala ya silaha waziwasilishe silaha hizo pamoja na nyaraka zake 
katika vituo vya karibu vya Polisi kwa ajili ya uhakiki.
Imetolewa:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni