Zaidi ya wilaya 81 kuongezewa usikivu wa redio ya Taifa
————————–
Zaidi
ya Wilaya 81 ambazo zimekuwa hazipati usikivu wa redio ya Taifa nchini
kuongezewa usikivu kwa mwaka wa fedha 2016/17 na kuendelea.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Nnauye leo Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nachingwea
Mhe. Hasani Eliasi Masala juu ya kutokusikika redio ya Taifa katika
jimbo lake.
Aidha
Mhe. Nape amesema kuwa kutosikika kwa redio ya Taifa katika Wilaya hiyo
kumetokana na uchakavu wa mitambo, lakini kwa hivi sasa eneo la
Nachingwea Mjini linapata matangazo ya redio ya Taifa kwa kutumia
mitambo miwili midogo ya Redio-FM ya TBC-FM na mtambo wa TBC-Taifa.
“Nia
ya Serikali ni kufunga mitambo mipya na ya kisasa ya FM yenye nguvu
kubwa ya kilowati 2 ambao utakuwa na uwezo wa kurusha matangazo
yatakayowafikia wananchi sehemu mbali mbali nchi nzima,” alifafanua Mhe.
Nape.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, tathmini iliyofanyika kubaini usikivu wa redio ya
Taifa nchini umeonyesha kuwa jumla ya wilaya 81 hazina usikivu mzuri wa
redio ya Taifa kutokana na uchakavu wa mitambo.
Aidha
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imejipanga kufunga
mitambo mipya, sambamba na ukarabati wa majengo ya mitambo, ofisi na
miundo mbinu mbalimbali kuanzia mwaka wa fedha 2016/2017 na kuendelea
kwa kuanza na Mikoa iliyopo pembezoni ili kuboresha usikivu ikiwezekana
isikike mpaka nchi jirani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni