Waziri Mkuu ahagiza wakuu wa Wilaya na Mikoa kutembelea Vijijini ili kujua matatizo ya wananchi.
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa 
ameagiza wakuu wa wilaya na mikoa kufanya ziara katika maeneo yao hasa 
vijijini ili kujua matatizo ya wananchi wao kwa ukaribu na kuyapatia 
ufumbuzi.
Mhe.Majaliwa ameyasema hayo leo 
hii Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa 
walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda 
kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa 
 wakuu wa mikoa na wilaya waache kukaa maofisini mwao badala yake 
watembelee wananchi na hasa wale wa hali ya chini ili kujua matatizo yao
 ya Ardhi na kupatia ufumbuzi migogoro ya wafugaji na wakulima.
Pia Mhe.Majaliwa amewasisitiza 
wakuu hao kutambua kwamba majukumu waliyonayo ni makubwa na wananchi 
wana mategemeo makubwa juu yao na hivyo ni  budi wakatekeleza wajibu wao
 na kuhakikisha watanzania wanapata huduma zote za muhimu kwa kutumia 
elimu, uwezo, uadilifu, uaminifu na uwajibikaji walionao ili kufanikisha
 maendeleo kwa wananchi.
Aliongeza kuwa wakuu hao wana 
jukumu kubwa la kusimamia pesa za serikali pesa za miradi zinakokwenda 
katika halmashauri za wilaya zao na kukazia kuwa Serikali haitasita 
kuchukua hatua kwa yeyote ambaye hatofanya kazi zake kikamilifu.
Waziri mkuu amewaagiza wakuu wa 
Mikoa kushirikiana kwa karibu na wakuu wa Wilaya ili kutafuta ufumbuzi 
wa matatizo ya maeneo yao kwani wananchi wana kiu ya maendeleo katika 
maeneo yao.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni