WAZIRI MKUU KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC BOTSWANA
WAZIRI
 MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumatatu, Juni 27, 2016) 
kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi
 na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini  mwa Afrika wa Double Troika ya Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit)   utakaofanyika kesho (Jumanne, Juni 28, 2016).
Mhe. 
Waziri Mkuu anamuwakilisha Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye 
mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha 
Gaborone (GICC).
Mkutano
 huo utafunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Botswana Mhe. Lt. Jen. Seretse 
Khama Ian Khama ambaye ni SADC, utajadili hali ya siasa, ulinzi na 
usalama nchini Lesotho. Mkutano huu   utatanguliwa na Mkutano wa 
Makatibu Wakuu ambao utafanyika leo (Jumatatu, 27 Juni, 2016).
Pia 
mkutano huo utahudhuriwa na Marais wa Afrika Kusini, Mwenyekiti 
aliyetoka (outgoing chair) wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Mhe. 
Jacob Zuma , Mhe. Jacinto Filipe Nyusi, Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji na 
Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
Wengine
 ni Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland ambaye ni Makamu Mwenyekiti 
wa SADC, Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti 
anayeondoka wa SADC.
Waziri
 Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika 
Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo 
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Aziz Mlima na 
Maofisa wengine waandamizi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni