HIVI NDIVYO MASHABIKI WALIVYOVUNJA GETI LA UWANJA WA TAIFA WAKILAZIMISHA KUINGIA...
Mashabiki
wamewazidi nguvu na kuvunja geti la upande mmoja wa Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam wakilazimisha kuingia ndani ili kushuhudia mechi ya
Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe.
Hii
ilitokea baada ya mashabiki hao kutakiwa kuondoka katika enero hilo kwa
kuwa tayari idadi ya mashabiki kwenye Uwanja wa Taifa unaochukua
mashabiki 60,000 ilikuwa imetosha. Kiingilio ni bure baada ya uongozi wa
Yanga kupitisha hilo.
Jeshi
la Polisi Tanzania limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya
mashabiki wanaotaka kuingia kwenye Uwanja wa Taifa licha ya kwamba
hakuna nafasi.
Tayari mageti yamefungwa, lakini mashabiki walitaka kuingia zaidi ya hapo licha ya maelekezo ya polisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni