JAMII imeshauriwa kubadilisha mfumo wa kupenda kukaa nje ya nyumba zao kuepuka kupata maambukizo ya ugonjwa wa malaria
Na  Masanja Mabula –Pemba
———————————-
JAMII imeshauriwa kubadilisha 
mfumo wa kupenda kukaa nje ya nyumba zao kwa ajili ya mazungumzo hasa 
nyakati za usiku ili kuepuka kupata maambukizo ya ugonjwa wa malaria .
Mkuu wa kitengo cha 
kudhibiti ugonjwa wa malaria Pemba Bakar Omar Khatib alitoa ushauri huo 
wakati akizungumza na maafisa wa Wizara ya afya kutoka Wilaya ya 
Micheweni na Wete kwenye  mkutano wa uhamasishaji zoezi la utoaji wa 
vyandarua  vilivyotiwa dawa uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha 
uwalimu Benjamini Mkapa.
Amesema kwamba utafiti 
uliofanywa na wataalamu wa kitengo hicho umebaini kwamba  mbu 
anayesababisha malaria hupenda kukaa nje ya nyumba na kwamba  njia ya 
kukabiliana na ugonjwa huo ni kwa jamii kuachana na tabia ya kukaa nje 
kufanya mazungumzo .
“Mbu anayesababisha malaria nao 
ni wajanja wanapenda kukaa nje , hivyo ili kukabioliana na ugonjwa huu ,
 ni vyema jamii kubadilisha mfumo wa kukaa ya nje ya nyumba zao kwa 
ajili ya mazungumzo ”alifahamisha.
Aidha amesema kwamba kutokana na
 hali hiyo , walio katika hatari   ya kupata maambulizi ya ugonjwa huo 
 zaidi ni watu wazima kuliko watoto kwani ndiyo wanaopenda kukaa nje , 
hususani kwa  kuangalia TV na mazungumzo .
Nao washiriki wa kikioa hicho 
wamekishauri kitengo hicho kuzungumza na makampuni ya simu za mikononi 
ili yatumike kusambaza ujumbe ka wamiliki wa simu unaotambulisha 
matumizi sahihi ya vyandarua .
Juma Shaame Salim kutoka mamlaka
 ya usimamizi wa mazingira Wilaya ya Wete , alisema utaratibu huo 
utasaidia kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa wakati muafaka kutokana na 
idadi kubwa ya wananchi wanamiliki ya simu za mikononi 
“Kutokana umuhimu wa suala hili 
,  ni vyema kitengo hichi kuzungumza na makampuni wa simu za mikononi 
ili yasaidie kueneza ujumbe kwani wananchi wengi wanamiliki simu za 
mikononi ”alishauri .
Naye Ali Rajabu kutoka Wilaya ya
 Micheweni akichangia kaatika mkutano huo aliomba kitengo kuandaa sheria
 ndogo ndogo ambazo zitatumika akuwabana wananchi ambao wanavitumia 
vyandarua kinyume na ilivyokusudiwa 
Alifahamisha kwamba 
baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo vyandarua vimezungushiwa bustani huku 
baadhi wakivitumia kwa ajili ya uvuvi wa dagaa , jambo ambalo  
linakwamisha ufanisi wamapambano dhidin ya malaria .
Akifunga kikao hicho 
kwa niaba ya Afisa Mdhamini wizara ya afya pemba , dk Harouk Khalifan 
hamad alisema mapambano dhidi ya malaria yanahitaji nguvu ya pamoja 
kutoka wadau na wananchi wote .
katika zoezi la 
ugawaji wa vyandarua kwa msimu huu jumla ya wananchi laki mbili hasini 
na tisa elfu na mia nane thelethini na sita (259,836) ambapo 
walioandikishwa ni wananchi laki nne sitini na saba elfu nan mia saba na
 sitini na tatu (467,763) kwa kisiwa cha Pemba .
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni