TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI,
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAMKO
 KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI, PAMOJA NA MLIPUKO WA
 UGONJWA WILAYANI CHEMBA NA KONDOA, MKOANI DODOMA,  LILILOTOLEWA NA MHE.
 UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA
 WATOTO, TAREHE 27 JUNI, 2016
Wizara ya Afya, Maendeleo ya 
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inaendelea na utaratibu wa kutoa tahadhari
 kwa wananchi na maelekezo ya hatua za kuchukua katika kukabiliana na 
mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu. Huu ni mwendelezo wa utoaji wa 
taarifa ya kila wiki, kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu kama tulivyoahidi. 
Hadi kufikia tarehe 26 Juni 2016, jumla ya wagonjwa 22,185 wametolewa 
taarifa, na kati yao, watu wapatao 344 wamepoteza maisha, tangu ugonjwa 
huu uliporipotiwa mnamo mwezi Agosti 2015.
Takwimu zinaonyesha kuwa, katika 
wiki hii inayoishia   tarehe 26 Juni 2016, idadi ya wagonjwa wa 
Kipindupindu walioripotiwa ni 365 na hakuna aliyepoteza maisha.  Idadi 
kubwa ya wagonjwa hawa walitolewa taarifa kutoka wilaya ya Ukerewe (316)
 ambapo imejumlisha wagonjwa kutoka tarehe 7 Aprili hadi tarehe 21 Juni 
2016. Hivyo, wagonjwa wa Kipindupindu wapya walioumwa kati ya 20 hadi 26
 Juni 2016 pekee ni takriban 49. Takwimu hii inaashiria kuwa wagonjwa 
wameongezeka kidogo ikilinganishwa na wiki iliyotangulia, ambapo 
kulikuwa na wagonjwa 46 na vifo viwili. Mikoa iliyoripoti ugonjwa wa 
Kipindupindu wiki hii ni Morogoro (Morogoro mjini 15, Kilosa 9 na 
Mvomero 3), Mara (Tarime vijijini 18), Mwanza (Ukerewe 319) na Arusha 
(Arusha Vijijini (1).
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni