Bunge limepitisha muswada wa marekebisha ya sheria ya ununuzi wa umma wa mwaka 2016
——————–
Bunge
 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha muswada wa 
marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016 wenye lengo la 
kupunguza gharama na muda wa mchakato wa manunuzi Serikalini.
Marekebisho
 hayo yametokana na gharama kubwa ambayo Serikali imekuwa ikitumia 
kutokana na huduma na Bidhaa zinazonunuliwa na Serikali kuwa za juu 
ikilinganishwa na bei ya wastani ya soko.
“Muswada
 wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016 una lengo la 
kuongeza ufanisi katika ununuzi wa Umma kwa kuondoa mapungufu yaliyopo 
katika Sheria ya sasa kwa kupunguza gharama na muda wa michakato ya 
ununuzi, kutoa upendeleo kwa kampuni za ndani, vikundi maalum, malighafi
 na bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na kuweka viwango mahsusi kwa 
bidhaa zitakazotumiwa na Serikali,” alifafanua Mwanasheria Mkuu wa 
Serikali Mhe. George Masaju.
Mhe. 
Masaju ameendelea kwa kusema kuwa sheria hiyo imeweka kifungu cha 
dharura  ili kuwezesha vitu vya kuokoa uhai na vinginevyo kununuliwa kwa
 dharura pindi inapobidi.
Kwa 
upande wake Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni yeye ameiomba 
Serikali kuruhusu kununua vifaa tiba vilivyotumika ambavyo muda wake wa 
kutumia hauna mwisho, kwa mfano vitanda vya kujifungulia  ili kupunguza 
gharama ya kununua vitanda vipya na kuweza kununua vitanda vingi kwa 
wakati mmoja.
Aidha
 Mhe. Jitu ameiomba Serikali kuirudisha tena Sheria hiyo Bungeni baada 
ya mwaka mmoja ili kufanyiwa marekebisho na kuziba mianya yote ambayo 
itakuwa imebainika mara baada ya utekelezaji wake kuanza.
Muswada
 wa marekebisho ya sheria hiyo yanasubiri kusainiwa na Rais wa Jamhuri 
ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli ili kuanza utekelezaji 
wake.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni