Waziri Nape Nnauye azindua Studio ya Redio ya Jamii katika Chuo Kikuu Huria Tanzania.
Waziri
 wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa 
ameongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. 
Elifas Bisanda kwenda kuzindua Studio ndani ya Chuo hicho 27 Juni, 2016 
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
 wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikata
 utepe wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network
 of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
 wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) 
akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa toka Shirika la 
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira 
Rodrigues wakati wa Uzinduzi wa ‘’Community Media Network of Tanzania 
(COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) 
akiwa ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania 
(COMNET)’’ akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari mara 
baada ya kuizindua rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
 wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa 
ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 
akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua 
rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
……………………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa 
na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amezindua studio ya redio ya jamii ya 
‘Community Media Network of Tanzania’ (COMNET)   katika Chuo kuku Huria(
 OUT )  itakayotumika kusambaza habari maeneo yenye uhaba wa redio.
Uzinduzi huo umefanyika   leo 
jijini Dar es Salaam,ambapo Mhe. Waziri  amesema kuwa studio hiyo 
itasaidia  idadi kubwa ya wanachi wanaoishi vijijini kupata habari 
kutoka Serikalini na kutoa mrejesho wa kile watakachosikia kwa urahisi.
“Ni Studio muhimu kwa ajili ya 
kusambaza demokrasia  kwa watu hasa wale waliopo vijijini kwa vile redio
 nyingi bado hazijawafikia”Alisema Mhe.Nape.
Aidha amewataka wanafunzi wa 
taaluma ya uandishi wa habari na  mawasiliano kwa umma katika  chuo  
hicho kutumia studio hiyo kujifunza zaidi kwa vitendo na kuzingatia 
maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zenye ukweli kutoka 
vyanzo sahihi ili kutoa ujumbe wenye manufaa mazuri kwa jamii.
Kwa upande wake Makamu mkuu wa 
Chuo hicho Prof. Elifas Bisanda amesema studio hiyo imeanzishwa kwa 
ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na 
Utamaduni(UNESCO)  kwa lengo kutoa elimu kwa jamii ambayo imekuwa 
haipati habari kwa urahisi.
Amewataka wanahabari na wananchi 
kwa ujumla   kufikisha habari katika studio hizo kwa kuwa inatumia njia 
ya haraka na rahisi katika kufikisha ujumbe kwa kushirikiana na redio 
mbalimbali za jamii.
 Naye mwakilishi kutoka Shirika la
 umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi,na Utamaduni(UNESCO) 
Bi. Zulimira Rodrigues  amesema studio ya redio ya ‘Community’ ipo kwa 
ajili ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo ya wanawake na vijana 
ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Mpaka sasa Shirika hilo 
limefanikiwa kuanzisha redio za jamii katika baadhi ya mikoa ya Tanzania
 bara ambayo ni Mwanza,Arusha na Tanga na katika baadhi ya maeneo ya 
Unguja na Pemba.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni