Mashine za tiketi za kieletroniki kuanza kutumika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.
Kaimu
 Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari 
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisisitiza jambo wakati 
alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji  wa mashine za tiketi 
zakieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mhandisi
 kutoka kampuni ya B.C.E.G ya China Bw. Xiong (kushoto) akifafanua jambo
 kwa Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya 
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge(kulia) kuhusu 
mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kutumika kuingia katika
 Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mtaalamu
 wa Mashine za tiketi za kieletroniki kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew
 Emmanuel (kushoto) akimuelekeza jinsi ya kutumia moja ya mashine hizo 
Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari 
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipotembelea kuangalia 
maendeleo ya uwekaji wa mashine hizo  uwanjani hapo Leo Juni 27,2016.
Mtaalamu
 kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel akirekebisha moja ya 
mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia
 katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.
Baadhi
 ya wananchi wakijaribu kutumia mashine ya tiketi za kieletroniki 
zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi 
karibuni.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni