Rais Magufuli Awataka wakuu wa Wilaya na mikoa kuchapa kazi.
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa wilaya na mikoa
kuchapa kazi kwa bidii kwani viongozi hao ndio wawakilishi wa wananchi
wa vijijini.
Mhe.Rais Magufuli ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu
wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu
wa mikoa yao.
Rais Magufuli pia amewataka
viongozi hao kufanya kazi na kutimiza majukumu yao kwani wananchi wana
changamoto nyingi,na wao waende kutatua matatizo ya wananchi walio
maskini.
Aidha amewataka viongozi hao
kutokuwa chanzo cha kutengeneza matatizo katika jamii na hivyo wasimamie
haki na ukweli,wasiwe wala rushwa,wazingatie maadili na kuwatumikia
wananchi wote bila kujali itikadi za vyama zao,dini au kabila uku
akiwataka kutekeleza waliyohaidi kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.
Pia amewataka viongozi hao kuweke
mkazo katika kutatua kero za wananchi na kuwataka kutimiza kwa vitendo
kwa kushirikiana na viongozi watakaowakuta katika maeneo yao
waliyopangiwa.
Hata hivyo amewataka viongozi hao
kusimamia mapato ya Serikali katika miradi yote kwenye maeneo yao ili
kuhakikisha serikali inapata kodi ambayo itasaidia katika maendeleo ya
Taifa hili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni