PROF. MBARAWA AKAGUA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE DODOMA
Waziri
 wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa 
maelekezo kwa Mkandarasi Kampuni ya Chico, anayefanya upanuzi wa njia ya
 kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa ndege wa Dodoma.
Ujenzi
 wa Barabara ya Kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa ndege wa Dodoma 
ukiendelea. Ujenzi huo kwa kiwango cha lami unatarajiwa kukamilika 
katika kipindi cha miezi miwili.
Waziri
 wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa 
maelekezo kwa Meneja wa Miradi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania 
(TAA) Eng. Mbila Mdemu ( wa pili kulia), wakati alipokagua maendeleo ya 
mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma.
Meneja
 wa Miradi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. Mbila 
Mdemu, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, 
Profesa Makame Mbarawa, alipokagua maendeleo ya upanuzi wa Uwanja wa 
Ndege wa Dodoma.
————————————————————-
Waziri
 wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi
 miwili kwa mkandarasi Chicco anaefanya upanuzi wa njia ya kuruka na 
kutua ndege katika uwanja wa ndege wa dodoma kuhakikisha kuwa ujenzi huo
 unakamilika.
Akizungumza
 mara baada ya kukagua kazi ya upanuzi wa uwanja huo, Prof. Mbarawa 
amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa ujenzi wa uwanja huo 
unafanyika kwa kuzingatia viwango vilivyokubalika katika mkataba na 
kuukabidhi kwa wakati.
“Hakikisheni
 upanuzi huu unakamilika kwa wakati ili kuupa hadhi inayostahili uwanja 
wa ndege wa Dodoma,hasa mkizingatia umuhimu wake kitaifa’, amesema Prof.
 Mbarawa.
Naye 
Mkandarasi anaejenga uwanja huo amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa
 atahakikisha ujenzi wake unazingatia viwango na kuukabidhi katika muda 
uliokubalika kimkataba.
Zaidi
 ya shilingi bilioni 11.8  zinatarajiwa kutumia katika upanuzi huo na 
hivyo kuwezesha ndege nyingi zaidi kutumia uwanja huo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni