UFAFANUZI KUHUSU USHIRIKI WA YOUNG AFRICANS
Shirikisho
 la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limekuwa likitoa kila aina ya msaasa 
uliowezekana kuisaidia klabu za Young Africans na Azam ambazo 
ziliwakilisha nchi katika mashindanmo ya kimataifa. Kwa upande wa Young 
Africans awali walishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na upande wa Azam 
ilishiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mtakumbuka,
 Azam FC ilitolewa na Esperance ya Tunisia katika michuano hiyo na kwa 
upande wa Young Africans iliposhindwa kufuzu kwa hatua ya Nane Bora ya 
Ligi ya Mabingwa Afrika, ikashushwa na kucheza na Esperanca Sagrada ya 
Angola na kuitoa hivyo kufuzu kwa hatua ya Nane Bora ya Kombe la 
Shirikisho au kwa lugha nyingine, hatua ya Makundi. TFF ikaendelea 
kuisaidia Young Africans kuhakikisha inashiriki vema katika mashindano 
hayo.
Sasa,
 Aprili 21, 2016 Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilitoa 
waraka kwa timu zilizokuwa zinacheza kuwania kuingia hatua ya Makundi 
(Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho) kupeleka majina ya 
maofisa watakaohudhuria warsha ya namna ya kuratibu mechi hizo kuelekea 
fainali. Kadhalika walitakiwa kupeleka vivuli (photocopies) vya hati zao
 za kusafiria.
Maofisa
 walihitajika ni meneja wa timu, daktari wa timu na ofisa habari wa 
timu. Taarifa hiyo ilikuja kabla ya Young Africans kucheza na Esperanca 
ya Angola. TFF iliwaataarifu Young Africans kwa kuwataka kutuma nyaraka 
hizo kati ya Aprili 26 na Aprili 28, 2016.
Lengo
 la warsha ilikuwa ni kujadili maswala ya uratibu, ufundi, udhamini na 
kanuni za mashindano. CAF ilijitolea kugharamia usafiri, malazi na 
gharama zote kwa watu watatu kutoka Young Africans SC.
Taarifa
 hizi na hata ukumbusho (reminders) zilipelekwa kwa baruapepe, simu na 
hata kuonana ana kwa ana kwa Katibu Mkuu wa Young Africans, Ofisa Habari
 na Viongozi wengine wa klabu.
Maofisa
 wa TFF kwa nyakati tofauti tofauti waliwasihi Young Africans na pia 
kuwakumbusha kutuma majina CAF na vivuli vya hati hati ya kusafiria, 
lakini kwa sababu wanazoweza kuzielezea wenyewe kwa nini hawakupeleka 
majina.
Mei 
22, 2016 ikiwa ni siku mbili kabla ya warsha kuanza hapo Mei 24, 2016, 
Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Bwana Baraka Deusdedit alituma 
majina CAF yakiwa hayana vivuli yaani photocopies vya hati ya kusafiria.
Siku 
moja kabla ya washiriki kuanza kuwasili Cairo, Misri, Kaimu Katibu Mkuu 
wa Young Africans alituma nyaraka kama zilivyotakiwa na wakatumiwa 
tiketi tatu (3) na CAF. Pamoja na tiketi kuletwa Young Africans bado 
watu hao hawakusafiri wakidai klabu haijatoa ruhusa.
Maofisa
 wa TFF wamekuwa wakifanya kazi mpaka muda wa ziada wakiwa na Kaimu 
Katibu Mkuu wa Young Africans, Baraka Deusdedit ili timu iweze kushiriki
 vema pamoja na upungufu wa kiutawala ndani ya sekretarieti yake 
yanayojidhihirisha wazi.
Masuala yote yanayolalamikiwa na Ofisa Habari wa Young Africans, yaliyotolewa kwa timu zote kwenye semina ya Cairo, Misri.
TFF 
itaendelea kuvitembelea kusaidia klabu kujenga weledi kupitia mradi wa 
leseni za klabu na vilevile kuratibu ushiriki wa mashindano mbalimbali.
Hata 
hivyo, TFF haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa maofisa wa klabu 
wanaochafua jina la shirikisho ili kuficha madhaifu yao ya kiutawala 
(Administrative inefficiencies).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni