MBUNGE TUNDU LISSU AWEKWA LUMANDE BAADA YA KUKOSA DHAMANA
Na Mwandishi wetu, Dar
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema),Tundu
Lissu amewekwa lumande baada ya kukosa dhamana.
Kukosa dhamana hiyo kunafuatia kwa Mbunge Lissu
kuripoti katika kituo cha polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam leo hii kwa
ajili ya kuhojiwa na jeshi hilo kuhusu kauli aliyoitoa jana baada ya kutoka
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu kuhusiana na
maneno mengine ambayo ameyaandika kupitia mitandao ya kijamii yanayodaiwa kuwa
ni ya uchochezi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam leo,Mbunge wa Arusha mjini,Godbles Lema amekili kuwa Lissu amewekwa lumande kwa kukosa dhamana na hataachiwa leo atalala lumande.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni