ENGLAND 'MAKELELE' WANG'OLEWA EURO NA ICELAND
Pamoja
na kutokuwa na mafanikio makubwa sana katika michuano ya kimataifa,
England ndiyo wanaongoza kwa kuwa na makelele mengi na leo, wameng’olewa
kwenye michuano ya Euro kwa kuchapwa mabao 2-1.
Mabao hayo 2-1 yametoka kwa Iceland ambayo awali ilionekana ni kibonde na isiyo na uwezo.
Lakini
imefanikiwa kuonyesha soka safi, ikitoka nyuma na kusawazisha halafu
ikafunga bao la pili. England walianza mapemaa kwa bao la penalti la
nahodha Wayne Rooney.
Lakini
mwisho, England wakatoka na kuacha gumzo kwani Iceland inakwenda nusu
fainali ikiwa iliingia katika michuano hiyo haipewi hata nafasi ya
kuvuka hatua ya makundi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni