WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKI MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Wizara
 ya Maliasili na Utalii itashiriki katikaMaonesho ya40 ya Biashara ya 
Kimataifa ya Dar es Salaam(SABASABA)kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 8
 Julai, 2016 katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere, Dar es Salaam.
Wizara
 itakuwa na washiriki kumi na sita (16) ambao ni Idara pamoja na Taasisi
 zake mbalimbali. Idara zitakazoshiriki ni Utalii, Wanyamapori, Mambo ya
 Kale na Misitu na Nyuki.
Kwa 
upande wa Taasisi ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Taifa cha 
Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka
 ya Hifadhi ya Ngorongoro,Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na 
Vyuo vya Wanyamapori (Mweka, Pasiansi na Likuyu Semaganga).
Taasisi
 nyingine ni Vyuo vya Misitu na Nyuki (Olmotonyi, FITI Moshi na Chuo cha
 Nyuki Tabora), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Wakala wa Mbegu za 
Miti, Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na 
Utalii.
Washiriki
 wote hao watakuwa kwenye banda moja la MALIASILI, Wizara inawakaribisha
 wananchi wote kwenye banda hilowaweze kujionea na kuelimika 
namambombalimbali yanayohusu Utalii,  Ufugaji wa Nyuki, Uhifadhi wa 
Misitu, Malikale na Wanyamapori.
Aidha,
 Wizara itatoa punguzo kwa watanzania kutembelea Hifadhi ya Taifa ya 
Mikumikwa gharama nafuu. Safari ya kwenda na kurudi kwa watoto itakua 
Tsh. 10,000 na watu wazima Tsh. 20,000. Safari ya kulala itakuwa Tsh. 
50,000.
Pia 
katika maonesho hayo itakuwepo fursa ya kuwaona wanyamapori hai 
mbalimbali kama vile Chui, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na 
SIMBA.
Kaulimbiu ya Maonesho hayo mwaka huu inasema“Tunaunganisha Uzalishaji wa Masoko”
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maliasili na Utalii
27 Juni, 2016.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni