SERENGETI BOYS YAONGOZA GOLI 3-0 DHIDI YA SECHELLES UWANJA WA TAIFA,MPIRA UNAENDELEA.
Mpira umeanza kwa kasi na katika dakika 10 za mwanzo Serengeti Boys 
wanaonekana kutawala mpira na katika dakika ya 15 Nickson Kibabage anaiandikia Serengeti goli la kwanza akitumia maridadi mguu wake kushoto na kutinga nyavuni.
 
Dakika ya 22, Ibrahim Ally anaiandikia Stars goli la pili ikiwa ni 
shambulizi lililoanzia katikati ya uwanja.Mpira  umeonekana kuchezwa 
upande mmoja na Serengeti kukosa nafasi nyingi za  wazi.Mpira ni 
mapumziko na Serengeti wanatoka wakiwa mbele kwa goli 2.
Kipindi cha pil kimeanza na timu zote kuwa makini ambapo dakika ya 60, Ally Msengi anaiandikia Serengeti goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Shelisheli kuushika ndani ya 18 na mwamuzi kuamuru penati.
Mchezo kati ya Serengeti Boys na Sechelles unaopigwa hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza kwa bao 3-0.

Wachezaji wa timu ya Serengeti Boys wakishangilia mara baada ya kupata goli. 
Mchezaji
 wa timu ya Serengeti Boys Rashid Mohamed Chambo akimchomoka  mchezaji 
wa timu ya Sechelles,katika mchezo wao unaopigwa hivi sasa  uwanja wa 
Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza  bao 3-0. 
Mchezaji
 wa timu ya  Sechelles akiwa amelelala chini katika nginja ngija ya 
kusaka magoli dhidi ya timu ya Serengeti Boys ,katika mchezo wao 
unaofanyika hivi sasa uwanja wa  Taifa, hadi sasa Serengeti Boys 
inaongoza bao 3-0.
Picha kwa hisani ya Michuzi Blog
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni