MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA WAZIRI KUTOKA MALAYSIA NA MAKAMU WA RAIS WA TIGO AFRIKA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Waziri asiye
na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi
Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na
utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala ,Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri asiye na Wizara Maalum
katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa
kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na utekelezaji wa miradi
ya serikali Dk. Sri Idris Jala (kushoto) mara baada ya mazungumzo ,Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri asiye na Wizara Maalum katika
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo
kinachoshughulikia masuala ya utendaji
Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Makamu wa Rais wa Tigo Afrika Bi. Rachel Samren (Kushoto)
wakati Bi. Rachel Samren alipomtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake
Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Juni 2016.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa Tigo Afrika Bi. Rachel Samren wengine
pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kisheria
Bi. Sylvia Balwire na Bi. Halima Okash Afisa Uhusiano (wa kwanza
kushoto) Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Juni 2016.
——————————————————–
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameiomba
serikali ya MALAYSIA kujenga ofisi za ubalozi wake hapa
nchini ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
nchini ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Makamu
wa Rais ametoa kauli hiyo leo Juni 24, 2016 alipokutana na kufanya
mazungumzo Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA ambaye
aliongozana na Balozi wa MALAYSIA aliye na makazi yake jijini Nairobi Kenya, ISMAIL SALAM walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar Salaam.
aliongozana na Balozi wa MALAYSIA aliye na makazi yake jijini Nairobi Kenya, ISMAIL SALAM walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar Salaam.
Makamu
wa Rais amesema ujenzi wa ofisi za ubalozi huo hapa nchini utarahisisha
kwa kiasi kikubwa Watanzania wanaotaka kusafiri kwenda nchini
MALAYASIA kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za masomo na biashara kuliko hali ilivyo sasa ambapo ofisi za balozi hizo zipo Nairobi – Nchini KENYA.
MALAYASIA kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za masomo na biashara kuliko hali ilivyo sasa ambapo ofisi za balozi hizo zipo Nairobi – Nchini KENYA.
Kwa
upande wake Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA
amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi yake itaendelea
kuimarisha,kukuza
na kuendeleza mahusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia hasa uanzishaji wa ubalozi wake hapa nchini.
na kuendeleza mahusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia hasa uanzishaji wa ubalozi wake hapa nchini.
Hata
hivyo, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa Makubaliano ya
pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia ambayo
yatajikita katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, uchukuzi na biashara.
yatajikita katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, uchukuzi na biashara.
Wakati
huo huo, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN pia amekutana Makamu wa
Rais wa TIGO – Afrika RACHEL SAMREN ambapo wamezungumzia masuala
mbalimbali ikiwemo namna kampuni hiyo itakavyosadia katika kuwawezesha wanawake kuondokana na umaskini hapa nchini.
mbalimbali ikiwemo namna kampuni hiyo itakavyosadia katika kuwawezesha wanawake kuondokana na umaskini hapa nchini.
Katika kuhakikisha taifa linaongeza ukusanyaji wa mapato,
Makamu wa Rais ameuhimiza uongozi wa kampuni ya Simu ya Tigo hapa nchini kuhakikisha
unalipa kodi kwa uwazi ili fedha hizo ziweze kusaidia serikali katika kuimarisha
utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni