MASHINDANO MAKUBWA YA KUHIFADHI QURAAN TUKUFU KUFANYIKA DIAMOND JUBILEE JUMAPILI HII
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quraan Tukufu, Sheikh Othman Ally Kaporo (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Mashindano hayo yatafanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Sheikh Mohammed Ally Hassan(kulia) na Sheikh AllySendo
![]() |
Abuzar Kholidi kutoka Tajikistan |
NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID MASHINDANO
ya Kimataifa ya Kusoma na Kuhifadhi Quraan, yanatarajiwa kufanyika
Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo
Juni 23, 2016, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo,
Sheikh Othman Ally Kaporo, amesema, mashindano hayo ambayo ni sehemu ya
kutekeleza ibadaya funga
ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, yatashirikisha wanazuoni kutoka mataifambalimbali Duniani.
ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, yatashirikisha wanazuoni kutoka mataifambalimbali Duniani.
“
Kwa wale watakaojaaliwa, wanaweza kufika kwenye msikiti wa Mtoro ulioko
Kariakoo, na kujionea jinsi vijana wadodo wanavyosoma Quraan, kila siku usiku, na Jumapili ndio mashindano yenyewe haswaa.’Alisema.

Katika
mkutano huo na waandishi wa habari, washindani watatu waliwaonyesha
waandishi umahiri wao wa kuhifadhi Quraan, miongoni mwao ni wanafunzi
wawili wenye umri wa miaka kati ya 8 na 10, Abuzar Kholidi kutoka
Tajikistan, na Ahmed Abdallah
kutoka Bangladesh. Kijana mwingine aliyeonyesha ufundiwa kuhifadhi Quraan Tukufu ni Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia.
kutoka Bangladesh. Kijana mwingine aliyeonyesha ufundiwa kuhifadhi Quraan Tukufu ni Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia.
Ahmed Abdallah kutoka Bangladesh
Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni