HABARI ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
Kocha
Mkuu wa timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Tanzania, Nasra
Juma ametangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Twiga
Stars.
Kikosi
hicho kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda Julai 15, 2016 kucheza mchezo
wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda ikiwa ni
mwaliko maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (Ferwafa).
Wakati
Ferwafa likiingiza mchezo huo wa Julai 17, 2016 kwenye orodha ya
michezo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira na Miguu la Kimataifa
(Fifa), lakini Mheshimiwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kuwa sehemu ya
burudani ya burudani mbele ya wageni wake ambao ni wakuu mbalimbali
wanaounda Umoja wa Nchi za Afrika (AU) ambao watakuwa na mkutano wao
nchini Rwanda.
Mbali
ya soka kama burudani, pia Rais Kagame atatumia mchezo huo kama hamasa
kwa wakuu wa nchi ili kutoa kipaumbele kwenye soka la wanawake ambako
kwa sasa ni ajira ambayo inakwenda sambamba na kuitikia wito wa
kupambana na changamoto za malengo ya millennia (MCC) ambayo pia
yanataka wanawake wapate nafasi.
Makipa:
- Fatma Omary
- Belina Julius
- Najiat Abbas
Walinzi:
- Stumai Abdallah
- Fatma Issa
- Anastazia Antony
- Happuness Henziron
- Maimuna Khamis
Viungo:
- Donisia Daniel
- Amina Ali
- Amina Ramadhani
- Fatuma Bashiri
- Wema Richard
- Fadhila Hamadi
- Mwajuma Abdallah
- Anna Hebron
- Sophia Mwasikili
Washambuaji:
- Tumaini Michael
- Johari Shaaban
- Fatma Idd
- Shelder Bonifdace Mafuru
- Asha Saada Rashid
- Mwanakhamisi Omar
…………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni