Watanzania Kumiliki hisa Katika Kampuni za Mawasiliano Hapa Nchini.
  —————————-
Serikali
 kufanya marekebisho ya Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kieletroniki 
ili kuwezesha watanzania kumiliki hisa zitakazouzwa na Kampuni za 
Mawasiliano kupitia soko la hisa.
Hayo
 yamesemwa leo Bungeni  Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. 
Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha Bungeni  muswada wa Sheria ya 
Fedha ya mwaka 2016. 
“Mhe.
 Naibu Spika, sehemu ya nne inapendekeza marekebisho katika sheria ya 
Posta na   Mawasiliano ya Kielektroniki, sura 306 kama ifuatavyo, kufuta
 kifungu cha 6(2d) na kukiandika upya ili kuweka sharti kwa kampuni za 
mawasiliano kuwasilisha Katiba ya Kampuni itakayothibitisha muundo wa 
umiliki wa hisa kama mojawapo ya taarifa zinazopaswa kuwasilishwa wakati
 wakuomba leseni,” alifafanua Mhe. Mpango.
Aidha
 Mhe. Mpango aliendelea kwa kusema kwamba, watoa huduma za Mawasiliano 
ya Kielektroniki watawekewa sharti la kuuza hisa zao kwa Umma na 
kusajili hisa zao katika soko la hisa Nchini Tanzania ili kutoa fursa 
kwa watanzaniai kununua hisa na kumiliki asilimia 25 ya Kampuni hizo.
Kutokana
 na marekebisho ya sheria hiyo, kampuni za huduma za Mawasiliano ya 
kielektroniki ambazo tayari zimesajiliwa hapa Nchini zitawajibika 
kujioredhesha katika soko la hisa na kuuza hisa zao ndani ya kipindi cha
 miezi sita kuanzia Julai 01, 2016.
Vile
 vile kampuni ambazo zitasajiliwa baada ya Julai 01, 2016 zitawajibika 
kuuza hisa zao na kujioredheshsha katika soko la hisa ndani ya kipindi 
cha Miaka miwili kuanzia Julai 01, 2016.
Kwa
 upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti  Mhe. 
Hawa Ghasia amesema kwamba kamati imekubaliana na marekebisho hayo aidha
 kamati inaishauri Serikali  kuweka tafsiri ya watanzania ili kuwezesha 
hisa hizo kuuzwa kwa watanzania  pekee na pia kuangalia suala la miezi 
sita kwa makampuni yaliyosajiliwa lisilete utata kwenye utekelezaji 
wake.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni