ZLATAN, MAN UNITED WAMALIZANA, ATATANGAZWA RASMI IJUMAA
Baada
ya kusubiriwa kwa muda mwingi, hatimaye Manchester United inatarajia
kumtangaza rasmi Zlatan Ibrahimovic kuwa mchezaji wake mpya.
Zlatan,34, atatangazwa Ijumaa hii kuwa mchezaji wa Man United iliyo chini ya Jose Mourinho.
Raia
huyo wa Sweden amemaliza mkataba wake na PSG ya Ufaransa ambako
alifanya vema baada ya maisha yake ya soka akiwa Ajax nchini Uholanzi
baadaye nchini Italia akiwa na Juventus, Inter Milan na AC Milan, pia
Barcelona ya Hispania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni