COCA COLA YAMPAISHA MWANAFUNZI WA SEKONDARI YA TIRAV KWENDA PARISI UFARANSA KWENYE KAMBI YA KIMATAIFA YA SIKU 5.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohammed Kiganja,akizungumza na waandishi wa habari,Dar es Salaam,leo kuhusu wazazi kutoa nafasi kwa watoto wao kutumia nafasi katika michezo mbalimbali ili kuibua vipaji vingi. Kushoto ni Meneja Chapa Msaidizi wa Kampuni ya Coca Cola, Mariam Senziga. Picha na Elisa Shunda
Meneja Chapa Msaidizi wa Kampuni ya Coca Cola, Mariam Senziga,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni ya Coca Cola kumdhamini Mwanafunzi wa Sekondari ya Tirav Said Bakari kuelekea jijini Parisi nchini Ufaransa kwenye kambi ya Kimataifa iliyoandaliwa na Kampuni ya Coca-Cola kwa ajili ya kuiwakilisha nchi ya Tanzania kupitia mashindano hayo.
Kocha wa Michezo wa Shule ya Sekondari ya Kibasila,Abel Mtweve,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo wakati ukiendelea katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo,jijini Dar es Salaam,jana.
Mshindi wa Mwaka jana wa Michuano ya Copa Coca
Cola Taifa , Said Bakari (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dr es
Salaam jana kuhusu kuchaguliwa kwenda katika kambi ya Kimataifa nchini Ufaransa
kwaajili ya kujifunza. Katikati ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania
(BMT), Mohammed Kiganja na Meneja Chapa Msaidizi wa Kampuni ya Coca Cola,
Mariam Senziga.
NA RAYMOND URIO, Dar
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limewataka wazazi kuwapatia
fursa watoto kushiriki michezo waitakayo ili waweze kufanya kitu wakipendacho
na kukuza vipaji walivyonavyo.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Mohammed Kiganja, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumuaga Mchezaji bora wa Copa Coca-Cola msimu uliopita, Said Bakari, anaye tarajiwa kuondoka leo kuelekea Ufaransa kwenye kambi ya Kimataifa iliyoandaliwa na Kampuni ya Coca-Cola kwa ajili ya kuiwakilisha nchi ya Tanzania kupitia mashindano hayo.

“Tunaamini kwenda kwenye nchini Ufaransa mjini Paris,
mchezaji huyu ataiwakilisha nchi yetu na tunaamini atajifunza mengi kwa
kubadilishana uzoefu na wenzake kutoka nchi mbalimbali, hivyo wazazi wawape
watoto nafasi kushiriki michezo na fani mbalimbali ili kuweza kukuza vipaji
walivyonavyo ” alisema Kingoja.
Alisema kuwa kupelekwa kwa kijana huyo katika kambi hiyo itaweza kulisaidia taifa kukuza vipaji vyake kupitia mbinu mbali mbali ambazo kijana huyo atafundishwa na wakufunzi mbali mbali pindi awapo katika kambi nchini humo.
"Tunaamini kijana huyu atakuwa ni chachu ya maendeleo ya mpira hapa nchini kwa vijana wenzake kwani kupitia mbinu atakazozipata huko Ufaransa mjini Paris ataweza kuja kuwafundisha wenzake na hatimaye kuongeza idadi ya wachezaji wenye uwezo mkubwa hapa nchini kama vile walivyo akina Sammata" alisema Kiganja.
Aidha Kaimu Meneja Msaidizi wa Bidhaa na Masoko wa kampuni hiyo,Mariam Senziga alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kudhamini michuano mbali mbali hapa nchini ili kukuza tasnia ya michezo ambayo huchangia kukua kwa uchumi.
Alisema Jamii ijitokeze katika kuwahamasisha waweze kushiriki katika michezo kwani wanaamini kwa hivi sasa sekta hiyo imekuwa na heshima tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma ambako ilikuwa imedharauliwa zaidi.
Kwa upande wake Mshindi huyo wa Copa Coca-Cola Msimu uliopita, Said Bakari alisema kuwa ataitumia kambi hiyo ili kuweza kuongeza kiwango chake na hatimaye awezekufikia ndoto alizojiwekea.
"Napenda niwaahidi Watanzania kwamba katika nafasi hii niliyoipata nitaenda kuitumia ipasavyo ili niweze kujifunza vitu vingi zaidi ambavyo nilikuwa sivijui na kuongeza ujuzi zaidi ya ule nilliokuwa nao sasa" alisema Musa.
Musa anatarajiwa kusafiri hii leo kuelekea katika kambi itakayoanza kesho hadi Julai 4 itakayofanyika huko Jouy-En-Josas nchini ufaransa mjini Paris ambako anatarajiwa kurudi Julai 5 baada ya mafunzo hayo kuisha.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni