MSWADA WA SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA WA MWAKA 2106
Katika
kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 117(9) ya
Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016; Kamati ya Bunge ya
Bajeti imepanga kufanya mkutano wa kusikiliza maoni ya wadau wote wa
masuala ya Ugavi (Public Hearing) kuhusu Muswada wa Sheria ya Manunuzi
ya Umma wa Mwaka 2016 (Public Procurement Act 2016) kabla Muswada huo haujapitishwa na Bunge kuwa Sheria.
Mkutano
huo wa kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) unatarajiwa kufanyika
siku ya Jumatatu Juni 27, 2016 Bungeni Dodoma kuanzia saaTanoAsubuhi
katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni – Dodoma.
Kwa
kuzingatia umuhimu wa Muswada huo, Kamati inawaalika wadau wote kufika
na kuwasilisha maoni yao mbele ya Kamati kabla kupelekwa katika hatua
nyingine. Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au
Barua pepe kwa anuani ifuatayo:
Katibuwa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P. 941,
DODOMA
Baruapepe: cna@bunge.go.tz
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni